Connect with us

African Football

Urusi 2018: Safari ya kufuzu kombe la dunia yaendelea

Urusi 2018: Safari ya kufuzu kombe la dunia yaendelea

Zambia na Msumbiji zimeanza vizuri safari yao ya kufika katika hatua ya makundi kufuzu katika fainali ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Zambia ikicheza jijini Khartoum siku ya Jumatano, iliwafunga wenyeji wao Sudan bao 1 kwa 0 na Msumbuji ikicheza nyumbani jijini Maputo iliifunga Gabon pia kwa bao 1 kwa 0.

Michuano hiyo inaendelea siku ya Alhamisi jioni katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Jijini Lome, Togo ni wenyeji wa Uganda kutoka Afrika Mashariki na mchuano mwingine unachezwa ni kati ya Burundi ambao wanawakaribisha jirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jijini Bujumbura.

Michuano ya marudiano itachezwa wiki ijayo na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi ili kuendelea na michuano ya kutafuta mataifa matano yatakayowakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo ya dunia.

Ratiba nyingine siku ya Alhamisi:

Namibia vs Guinea

Morocco vs Equatorial Guinea

Benin vs Burkina Faso

Siku ya Ijumaa Ijumaa Novemba 13 2015

Kenya vs Cape Verde

Madagascar vs Senegal

Liberia vs Ivory Coast

Comoros vs Ghana

Mauritania vs Tunisia

Niger vs Cameroon

Libya vs Rwanda

Angola vs Afrika Kusini

Siku ya Jumamosi Novemba 14 2015

Tanzania vs Algeria

Ethiopia vs Congo

Chad vs Misri

Bostwana vs Mali

More in African Football