Connect with us

Urusi 2018: Uganda na DRC waanza vizuri

Urusi 2018: Uganda na DRC waanza vizuri

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda, zilipata ushindi katika michuano yao ya kwanza kufuzu katika hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza katika kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Uganda ikicheza ugenini jijini Lome katika uwanja wa Stade de Kegue, iliifunga Togo bao 1 kwa 0 bao lililotiwa kimyani na Farouk Miya katika dakika ya 39 ya mchuano huo.

DRC alimaarufu kama Leopard, ikicheza ugenini katika uwanja wa Prince Louis Rwagasore jijini Bujumbura, iliishinda wenyeji wao Burundi mabao 3 kwa 2.

Mchuano huo ulichezwa huku mvua kubwa ikinyesha na DRC ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya tano ya mchuano huo ikifungwa na Yannick “Yala” Bolasie kabla ya Cedrick Amissi kuisawazishia Intamba Murugamba katika dakika 38 na kuongeza la pili dakika 83 ya mchuano huo huku Firmin Ndombe Mubele akifungia timu yake mabao 2 katika dakika ya 86 na 88.

Michuano ya marudiano itachezwa wiki ijayo na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi ili kuendelea na michuano ya kutafuta mataifa matano yatakayowakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo ya dunia.

Matokeo mengine:

Namibia 0 vs Guinea 1

Morocco 2 vs Equatorial Guinea 0

Benin 2 vs Burkina Faso 1

Siku ya Ijumaa Ijumaa Novemba 13 2015

Kenya vs Cape Verde

Madagascar vs Senegal

Liberia vs Ivory Coast

Comoros vs Ghana

Mauritania vs Tunisia

Niger vs Cameroon

Libya vs Rwanda

Angola vs Afrika Kusini

Siku ya Jumamosi Novemba 14 2015

Tanzania vs Algeria

Ethiopia vs Congo

Chad vs Misri

Bostwana vs Mali

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in