Connect with us

Vincent Enyeama astaafu kucheza soka la Kimataifa

Vincent Enyeama astaafu kucheza soka la Kimataifa

Kipa wa muda mrefu wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Vincent Enyeama ametangaza kuacha kuichezea timu yake ya taifa.

Hatua hii inakuja baada ya kufanya mashauriano na viongozi wakuu wa Shirikisho la soka nchini Nigeria NFF nchini Ubelgiji.

Hatua hii haijawashangaza wapenzi wa soka nchini Nigeria kwa sababu hivi karibuni alionekana kutofautiana na kocha Sunday Oliseh baada ya kumteua mshambuliaji wa CSKA Moscow Ahmed Musa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 anayecheza soka la kulipwa nchini Ufaransa katika klabu ya Lille mwaka uliopita baada ya kustaafu kwa beki Joseph Yobo alinukuliwa akisema muda wake wa kuachana na Nigeria ulikuwa haujafika.

Enyeama ametangaza uamuzi wake kupitia ukurasa wake Instagram.

Nimepigana vita vizuri kwa miaka 13.Nimemaliza kazi yangu.Nimelinda amani na kuimba wimbo wa taifa kwa hisia,” aliandika.

Mungu ibariki Nigeria.Kuanzia siku zijazo mimi sio nahodha wa Nigeria tena.Mimi sio kipa wa timu ya taifa, nimeachana na timu ya taifa,”.

Mwezi Juni, Nigeria ikicheza na Chad Enyeama aliichezea timu yake mchuano wake wa 101 na kuweka historia kwa kuichezea nchi yake kwa muda mrefu.

Kipa huyo atakumbukwa kuichezea Nigeria katika Makala matatu ya kombe la dunia na kuingoza nchi yake kushinda taji la Afrika mwaka 2013.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in