Connect with us

Waamuzi kutoka nchini Angola watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa hatua ya Makundi kati ya Young Africans ya Tanzania na Rayon Sports ya Rwanda utakaochezwa Mei 16,2018 Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo utakaochezwa saa 1 usiku mwamuzi wa katikati atakuwa Helder Martins Rodrigues De Carvalho akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba 1 Ivanildo Meirelles De O Sanche,mwamuzi msaidizi namba 2 Wilson Valdmiro Ntyamba,mwamuzi wa akiba Joao Amado Muanda Goma wakati Kamishna wa mchezo huo Abebe Solomon Gibresilassie kutokea Ethiopia,Mratibu wa mchezo anatokea Gabon Yoland Mavouroulou na Afisa Habari aliyeteuliwa na CAF kusimamia mchezo huo anatokea Tanzania Cliford Mario Ndimbo.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in CAF Confederations Cup