Connect with us

Wachambuzi wasema Bandari inahitaji wachezaji wenye uzoefu

Wachambuzi wasema Bandari inahitaji wachezaji wenye uzoefu

Wachambuzi wa soka Pwani ya Kenya wanasema, klabu ya Bandari FC iliyofuzu kuiwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya Shirikisho barani Afrika mwaka 2016 wanasema kuna umuhimu wa klabu hiyo kupata wachezaji wenye hadhi ya kucheza soka la Kimataifa.

Anthony Aroshee, mchambuzi wa soka na refarii wa zamani ameiambia soka25east.com kuwa licha ya Bandari FC kuwa na kocha mwenye uzoefu wa muda mrefu Twahir Muhiddin, inahitaji wachezaji watakaosaidia kuinua kiwango cha klabu hiyo.

Bandari ni lazima wafanye usajili wa kueleweka kuwapata wanasoka wenye uzoevu katika soka ya kimataifa,” alisema Aroshee.

Bandari FC yenye makao yake mjini Mombasa ilifuzu katika mashindano haya baada ya kuifunga Nakumatt FC mabao 4 kwa 2 katika fainali ya Gotv katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Mabao ya Bandari FC yalitiwa kimyani na Anthony Kimani dakika ya tano kipindi cha kwanza, huku Musa Mudde na George wakiongeza na kufikia 3 kwa 0 katika dakika 15 za kipindi cha kwanza.

Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza Bandari walikuwa na mabao 4 huku wapinzani wao wakiwa hawana kitu.

Kipindi cha pili, Nakumatt FC kupitia kwa Martin Imbalambala na Tyron Owino waliipa timu yao mabao mawili lakini hayakutosha kuiangusha Bandari.

Bandari FC sasa itamenyana na St.Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika hatua ya awali ya kusaka taji la Shirikisho mwezi Februari mwaka 2016.

Vlabu vingine kutoka Afrika Mashariki na Kati vlivyofuzu katika michuano hii ni pamoja na Police FC ya Rwanda, Atlabara ya Sudan Kusini, Khartoum FC ya Sudan, Atletico Olympic ya Burundi, Sport Club Villa ya Uganda, Azam ya Tanzania na CS Don Bosco ya DRC na Al-Ahly Shendi ya Sudan.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in