Connect with us

Rais wa Liberia George Weah, amesema anafikiri kuwajumuisha wachezaji wa timu ya taifa ya soka katika orodha ya wafanyikazi wa serikali, ili walipwe mshahara kila mwezi.

Iwapo atatekeleza hilo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa taifa la kwanza duniani kuwalipa wachezaji mshahara kila mwezi kama watumishi wa serikali.

Weah ambaye ni mchezaji wa zamani wa soka wa nchi yake, amekuwa akisema wachezaji wanajitoa na kufanya bidhaa kwa ajili ya taifa lao bila kupata chochote.

Hivi karibuni, timu taifa ya Liberia iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu fainali ya bara Afrika mwaka 2019 nchini Camerooon.

More in West Africa