Connect with us

Sadio Mane kutoka Senegal na Mohammed Salah kutoka Misri, ndio wachezaji pekee kutoka barani Afrika walioteuliwa katika orodha ya wachezaji 30 wanaowania taji la Ballon d’Or mwaka 2018.

Hata hivyo, orodha hiyo inatawaliwa na wachezaji wengi kutoka mabingwa wa taji la klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, ambayo imewakilishwa na wachezaji wanane.

Mshambuliaji kutoka Wales ,Gareth Bale na mshambuliaji kutoka Uingereza Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji wanaowania nafasi hiyo.

Eden Hazard kutoka Chelsea, Mohammed Salah wa Liverpool na Kevin de Bruyne anayechezea klabu ya Manchester City ni miongoni mwa wachezaji 11 kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Tuzo ya Ballon d’Or ilianza kutolewa mwaka 1956 na Gazeti la michezo nchini Ufaransa France Football.

Kati ya mwaka 2010 na 2015, Ballon d’Or, ilikubaliana na Shirikisho la soka duniani FIFA ,kutoa tuzo moja iliyopewa jina la FIFA Ballon d’Or.

Cristiano Ronaldo, alishinda tuzo hii mara mbili mfululizo mwaka 2016 na 2017.

Mshindi atatangazwa tarehe tatu mwezi Desemba jijini Paris.

More in