Connect with us

Wakaguzi wa Shirikisho la soka barani Arika CAF, watazuru nchini Cameoron siku ya Alhamisi kukagua utayari wa nchi hiyo kuwa mwenyeji wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika (AFCON) mwaka 2019.

Ukaguzi huu wa kwanza, ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka uliopita, ukaahirishwa baada ya kujiondoa kwa wakaguzi wa Kimataifa wa PricewaterhouseCoopers (PWC).

Ziara hiyo itachukua muda wa siku 12 kutembelea viwanja mbalimbali pamoja na kuthathmini hali ya hoteli kwa wageni.

Miongoni mwa viwanja ambavyo wakaguzi hao watazuru ni pamoja na uwanja wa Kimataifa wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde, uwanja wa Olembe na ule wa Bafoussam mjini Garoua.

Serikali nchini Cameroon inaendelea na ujenzi na ukarabati wa uwanja wa Limbe, Japoma na Doula.

Itakuwa mara ya kwanza kwa michuano hii kuwa na mataifa 24, badala ya 16 kama ambavyo imekuwa miaka iliyopita.

CAF inasema lengo ni kuleta ushindani katika michuano hii.

More in