Connect with us

Aliyekuwa Waziri wa Michezo nchini Kenya Hassan Wario amefikishwa Mahakamaji jijini Nairobi na kushatakiwa kwa madai ya ufisadi.

Wario na maafisa wengine wa zamani katika Wizara ya Michezo na Kamati ya Michezo ya Olimpiki, ameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya Shilingi Milioni 55, zilizotolewa na serikali, kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil.

Wario alikwenda kujisalimisha kwa Polisi hapo jana, na kukamatwa.

Noordin Haji, Mkuu wa Mashtaka ya Umma nchini humo anasema ana ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashataka wawili hao na maafisa wengine wa zamani waliohudumu katika Wizara ya Michezo.

Waziri huyo wa zamani wa Michezo, siku hizi ni Balozi wa Kenya nchini Austria.

Amekanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya Shilingi za nchi hiyo Milioni 1.

More in