Connect with us

Williamson ataja kikosi cha wachezaji wakulipwa

Williamson ataja kikosi cha wachezaji wakulipwa

Na Victor Abuso

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars Bobby Williamson amekitaja kikosi cha wachezaji 17 wanaosakata soka nje ya nchi katika maandalizi ya mchuano wa kufuzu kwa fainali za bara Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.

Harambee Stars inajiandaa kumenyana na Chipolopolo ya Zambia tarehe 6 mwezi ujao jijini Nairobi katika mchuano wa makundi.

Nahodha wa zamani wa Stars Dennis Oliech aliyekuwa anacheza soka nchini Ufaransa, Macdonald Mariga zamani akiichezea klabu ya Parma FC nchini Italia na Lawrence Olum anayecheza nchini Malaysia ni wachezaji wenye uzoefu walioitwa katika katika kikosi hicho.

Kikosi kamili:-Arnold Origi – Lillestrom (Norway), Brian Mandela – Maritzburg United (Afrika Kusini), David Owino – Zesco United (Zambia), David Ochieng (hana timu), Lawrence Olum – Kedah FA (Malaysia), Macdonald Mariga –(hana timu), Paul Were – (hana timu, Ayub Timbe – SK Lierse (Belgium), Clifton Miheso – VPS FC (Finland).

Wengine ni pamoja na, Anthony Akumu – Al Khartoum (Sudan), Victor Wanyama – Southampton FC (Uingereza ), Johanna Omollo – Royal Antwerp FC (Ubelgiji), Dennis Oliech – ((hana timu), Jacob Kelli – Nkana FC(Zambia), Allan Wanga – Azam FC (Tanzania).

Kenya ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa ufunguzi wa kundi lao la E dhidi ya Congo Brazaville huku Zambia nao wakitoka sare ya kutofungana na Guinea-Bissau.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in