Connect with us

 

Na Fredrick Nwaka ,Dar es Salaam.

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Yanga imeanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli ya Iringa.

Mechi hiyo imemalizika jioni hii katika Uwanja wa Taifa huku safu ya ushambuliaji ya Yanga ikishindwa kufurukuta.

Lipuli ilianza kufunga kupitia Seif Abdallah kabla ya Yanga kusawazisha kupitia mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

Mchezo huo ulikuwa wa kasi kipindi cha pili lakini timu zote zilishindwa kuongeza mabao.

Jumla ya mabao 19 yamefungwa katika michezo nane ya mzunguko wa kwanza

More in African Football