Connect with us

Yanga, Azam FC nguvu sawa ligi kuu Tanzania bara

Yanga, Azam FC nguvu sawa ligi kuu Tanzania bara

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga FC, walilazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Azam FC katika mchuano mgumu uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kuona lango la Azam katika dakika ya 47 kabla ya mapumziko kupitia bao la mshambuliaji wa Kimataifa kutoka nchini Zimbabwe Donald Ngoma.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kulisakama lango la mwenzake lakini Azam wakafanya mabadiliko na akaingia Kipre Herman Tchetche kutoka Cote Dvoire kuchukua nafasi ya Allan Wanga wa Kenya.

Tchetche aliisawazishia Azam FC dakika ya 82 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Farid Mussa na kufanya mambo kuwa sawa.

Dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchuano huo, Yanga walipata penalti iliyozua ugomvi kati ya timu hizo mbli lakini hakufanikiwa kuitia kimyani.

Kwa matokeo hayo, Yanga FC na Azam FC wote wana alama 16 baada ya michuano sita, wakifuatwa na Simba FC ina alama 15 na siku ya Jumamosi iliishinda Mbeya City bao 1 kwa 0.

Matokeo Kamili

Jumamosi Oktoba 17 2015

Young Africans

1

1

Azam FC

16:00

Majimaji

1

0

African Sports

16:00

Mbeya City

0

1

Simba SC

16:00

Ndanda FC

0

0

Toto Africans

16:00

Stand United

3

0

Tanzania Prisons

16:00

Coastal Union

0

1

Mtibwa Sugar

16:00

Mechi zijazo:

Jumapili Oktoba 18 2015

Mgambo JKT

vs

Kagera Sugar

16:00

Mwadui FC

vs

JKT Ruvu

16:00

Jumatano Oktoba 21 2015

Young Africans

vs

Toto Africans

16:30

Stand United

vs

Majimaji

16:30

JKT Ruvu

vs

Mtibwa Sugar

16:30

Tanzania Prisons

vs

Simba SC

16:30

Coastal Union

vs

Kagera Sugar

16:30

Alhamisi Oktoba 22 2015

Mwadui FC

vs

Mgambo JKT

16:30

Mbeya City

vs

African Sports

16:30

Ndanda FC

vs

Azam FC

16:30

 

 

 

 

 

 

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in