Connect with us

Yanga, Azam na Simba waendelea kupata ushindi

Yanga, Azam na Simba waendelea kupata ushindi

Ligi Kuu ya Tanzania bara iliendelea siku ya Jumatano huku mabingwa watetezi Yanga FC wakipata ushindi wa pili mfululizo.

Wanajwagani hao wakicheza mchuano wake wa pili katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam waliwashinda Tanzania Prisons mabao 3 kwa 0.

Mabingwa wa zamani nao waliendeleza ushindi wao baada ya kuishinda JKT Mgambo mabao 2 kwa 0.

Maji Maji ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Kagera Sugar, Mbeya City nao wakapata ushindi mkubwa wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya Ruvu Stars.

Matoke mengine, Azam FC 2 Stand United 0, Mtibwa Sugar 2 Toto Africans 1, Ndanda 1 Coastal Union 0 na Mwadui 2 African Sports 0.

Michuano hiyo inaendelea siku ya Jumamosi:-

JKT Mgambo-Maji Maji

Stand United-African Sports

Tanzania Prisons-Mbeya City

Young Africans-Ruvu Stars

Jumapili:

Mwadui- Azam

Mtibwa Sugar- Ndanda

Simba- Kagera Sugar

Costal Union-Toto Africans

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in