Connect with us

Klabu ya soka ya Yanga  Tanzania bara imepata alama tatu muhimu baada ya kuifunga Stand United bao 3-1 Jumatatu jioni katika mchuano wa ligi kuu katika uwanja wa Taifa jiji Dar es salaam.

Ushindi huu ni muhimu kwa klabu hiyo ambayo inafukuzana na vinara wa ligi Simba FC kutafuta ubingwa wa msimu huu.

Ushindi huu unaifanya Yanga kuwa na alama 46 sawa na Simba ambayo inaizidi kwa mabao.

Yanga imecheza mechi 21 huku Simba ikiwa imecheza mechi 20 hadi sasa .

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Azam FC kwa alama 44 ambayo imecheza mechi 22.

Azam ilipata alama tatu muhimu baada ya kuifunga Mbao FC kwa mabao 2-1.

More in