Connect with us

Mabingwa watetezi wa ligi Kuu Tanzania bara Yanga leo wanashuka kwenye uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya kuchuana na Tanzania Prisons huku mchezo huo ukiwa na shabaha kubwa mbili.

Yanga ni mabingwa  watetezi wa taji hilo lakini wako hatarini kupoteza ubingwa huo kwa watani wao wa jadi Simbva ambao wana alama 65. Yanga ina alama 48 ikiwa na mechi tano mkononi.

Katika mchezo huo ikiwa Yanga itashinda itaizuia Simba kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu na ikiwa itafungwa au kutoka sare itakuwa imeirahisishia Simba ubingwa wa msimu huu.

Kabla ya kuondoka kwenda Mbeya kwa mchezo huo Kocha mtarajiwa wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema timu yake haina budi kuachana na mbio za ubingwa wa ligi Kuu badala yake ielekeze macho yake kwenye mechi za hatua ya makundi ya taji la Shirikisho Afrika.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in