Connect with us

Klabu ya Yanga huenda ikamchukulia hatua za kinidhamu mchezaji wake Donald Ngoma baada ya kuondoka nchini na kuelekea Zimbabwe bila kuwasiliana na viongozi wake.

Mchezaji huyo yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha na amekosa mechi zaidi ya tano tangu msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulipoanza.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas ten amesema klabu yake inashangazwa na taarifa za mchezji huyo kuondoka nchini bila ruhusa ya uongozi, jambo linaloweza kutafsiriwa kuwa ni ukosefu wa nidhamu.

“Tumesikia kuwa ameondoka, kwenda Zimbabwe lakini sisi hatuna taarifa zake na wala uongozi haujui. Tunasubiri kuona lakini uongozi haujapendezwa na kitendo hiki,”amesema Dismas.

Ngoma, Thaba Kamusoko na Amiss Tambwe wako nje ya uwanja kwa sababu ya majeraha.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in