Connect with us

Yanga lazimisha sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Al Ahly

Yanga lazimisha sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Al Ahly

 

Klabu ya soka ya Yanga ya Tanzania imelazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Al Ahly ya Misri katika mchuano wa mzunguko wa pili kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika uliochezwa Jumamosi jioni katika uwanja wa taifa hapa jijini Dar es salaam.

Mabao yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo ulihudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa Yanga na mamia wa Al Ahly ambao walionekana wakiimba na kusherekea kipindi chote cha mchuano huo.

Al Ahly ilikuwa ya kwanza kupata bao na baadaye mabeki wake wakajichanganya na kujifunga na hivyo kuipa Yanga bao.

Matokeo haya yanamaanisha kuwa ni lazima Yanga wawafunge Al Ahly nyumbani ili kujikatia tiketi ya kufuzu katika hatua ya makundi kwa sababu ya bao la ugenini la wapinzani wao.

Mwaka 2009, Al Ahly iliishinda Yanga mabao 3 nyumbani na bao 1 ugenini na mwaka 2014 katika michuano ya Afrika, Yanga waliishinda Al Ahly nyumbani bao 1 kwa 0 lakini wakafungwa mabao 2 kwa 0.

Historia fupi ya Al Ahly

Ilianzishwa mwaka 1907.

Mwaka 2000 ilitajwa na Shirikisho la soka barani Afrika kama klabu ya Afrika ya Karne.

Mechi zake za nyumbani zinachezwa katika uwanja wa Cairo, jijini Cairo.

Klabu hii imeshinda ligi kuu nchini humo mara 37.

Mwaka 1977, walicheza na Bayern Munich ya Ujerumani na kuwashinda mabao 2 kwa 1.

Mwaka 2001 iliishinda Real Madrid ba 1 kwa 0.

Imeshinda taji la klabu bingwa barani Afrika mara 8, taji Moja la Shirikisho na mataji 6 ya Super Cup.

Inaingia katika historia ya soka duniani kwa kushinda mataji mengi zaidi yapatao 131 kwa jumla.

Al Ahly na Zamalek ndizo timu pekee nchini Misri ambazo hazijawahi kushushwa daraja.

Historia fupi ya Yanga FC

Mmoja wa Vlabu vikubwa nchini Tanzania, pamoja na Simba FC lakini hivi karibuni Azam FC imeanza kufahamika.

Iliazishwa mwaka 1935 na makao yake ni eneo la Jangwani Kariakoo, jijini Dar es salaam.

Imeshinda mataji mengi nchini Tanzania, ambayo ni 24 na ndio mabingwa watetezi.

Wameshiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika mara 9 na mwaka 1998 walifika katika hatua ya makundi.

Michuano ya kuwania taji la Shirikisho wameshiriki mara 3.

Wapinzani wao Simba, klabu ambayo ilianzishwa mwaka 1936 iliweka historia mwaka 1993 ilipofika katika fainali ya kuwania taji la Shirikisho la soka barani Afrika CAF na kufungwa na Stella Club ya Cote Dvoire.

Mwaka 2003, katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika iliiondoa mabingwa watetezi taji hilo wakati huo Zamalek ya Misri na kufuzu katika hatua ya makundi, chini ya kocha James Siang’a raia kutoka Kenya.

Kwa historia hii mashabiki wa soka nchini Tanzania wamekuwa wakisema kuwa Simba ina bahati nzuri katika michuano ya kitaifa.

Ratiba ya Michuano ya Klabu bingwa wikendi hii

Jumamosi Aprili 9 2016

  • ASEC Mimomas (Cote Dvoire) vs Al-Ahli Tripoli( Libya)-18:30
  • Zamalek (Misri) vs MO Bejaia (Algeria)-21:00
  • Wydad Casablanca (Morocco) vs TP mazembe (DRC)-21:30
  • Al-Merrikh (Sudan) vs ES Setif (Algeria):-20:00

Jumapili Aprili 10 2016

  • AS Vita Club (DRC) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
  • Enyimba (Nigeria) vs Etoile du Sahel (Tunisia)

Vlabu ambavyo vitaondolewa jatukahatuhii vitafuzu katika hatua ya mwondoano kutafuta ubingwa wa taji la Shirikisho.

Historia fupi ya TP Mazembe

Ilianzishwa mwaka 1939.

Makao makuu ni mjini Lubumbashi nchini DRC na uwanja wake wa nyumbani ni Stade TP Mazembe.

Ndio mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Afrika mwaka 2015.

Imeshinda mataji 5 ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 1967, 1968,2009,2010 na 2015.

Mwaka 2010 iliweka historia kwa kushiriki katika kombe la dunia baina ya vilabu iliyofanyika nchini Brazil na kufika katika hatua ya fainali lakini wakafungwa na InterMilan ya Italia kwa mabao 3 kwa 0.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in