Connect with us

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga leo imebanwa mbavu kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Prisons ilianza kwa kasi mchezo huo na kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia Jumanne Elfadhili kabla ya beki wa Prisons Eliuter Mpepo aliyejifunga dakika ya 42 akiwa katika harakati za kuokoa mpira golini kwake.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 21 na kukaa kwenye nafasi ya tatu ya msimamo ikiwa imecheza mechi kumi na moja.

Matokeo ya michezo mingine Stand United imeitandika Mbeya City mabao mawili kwa moja, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Ruvu Shooting imefungwa mabao 2-1 na Majimaji na Mbao FC imeibwaga Mwadui bao 1-0.

Kesho vinara wa Ligi hiyo Simba watachuana na Lipuli ya Iringa kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Baada ya michezo ya wiki hii ligi hiyo itasimama ili kupisha Tanzania bara ambayo itakuwa nchini Kenya kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in