Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga imepoteza pointi mbili muhimu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Majimaji.

Mchezo huo umechezwa kwenye Uwanja wa Majimaji Mjini Songea, Kusini Magharibi mwa Tanzania.

Majimaji ilitangulia kufunga kipindi cha kwanza kupitia Peter Mapunda na Mshambuliaji Donald Ngoma aliisawazishia Yanga dakika ya 79 kipindi cha Pili.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi tano na inandelea kubaki nyuma ya Mtibwa na Azam.

Mechi nyingine zilizopigwa Leo Mtibwa imeifunga Mbao FC Mabao 2-1.

Singida United ineichapa Stand United bao 1-0.

Prisons imetoka sare ya bila kufungan na Ndanda.

Kesho Simba itachuana na Mwadui jijini Dar es Salaam na Mjini Mbeya, Mbeya City itachuana na Njombe Mji.

More in East Africa