Connect with us

Yanga yaendelea kufanya vizuri ligi kuu Tanzania bara

Yanga yaendelea kufanya vizuri ligi kuu Tanzania bara

Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea katika viwanja mbalimbali nchini humo siku ya Jumatano.

Mabingwa watetezi Yanga waliendelea kuandikisha ushindi baada ya kuifunga Toto African mabao 4 kwa 1.

Simon Msuva alionesha ushupavu wake baada ya kuifungia timu yake mabao 2 huku nahodha Juma Abdul na mchezaji wa Kimataifa kutoka Burundi Hamis Tambwe wakifunga bao 1 kila mmoja.

Kwa matokeo hayo, Yanga wanaendelea kuongoza msururu wa ligi hiyo kwa alama 19 baada ya mechi saba hadi sasa.

Mabingwa wa zamani Simba nao wakicheza na Tanzania Prisons walifungwa bao 1 kwa 0, Stand United ikaifunga Majimaji FC mabao 3 kwa 0 huku Coastal Union ikiichabanga Kagera sugar bao 1 kwa 0.

Ligi kuu ya Tanzania bara imesitishwa hadi kumalizika kwa uchaguzi Mkuu siku ya Jumapili.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in