Connect with us

Yanga imeanza vizuri mechi ya hatua ya mwisho ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitandika Welatya Dicha ya Ethiopia kwa mabao 2-0.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na viungo Raphael daud na Emanuel Martin katika kila kipindi cha mchezo.

Kwa matokeo hayo Welatya Dicha inahitaji ushindi wa mabao 3-0 na zaidi ili kutinga hatua makundi ya michuano hiyo ya pili kwa umashuhuri kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Akizungumza baada ya mchezo huo nahodha wa Yanga, Nadir Haroub amesema timu yake ilitengeneza nafasi nyingi lakini haikuzitumia.

“Tumecheza vizuri lakini hatujatumia sana nafasi tulizopata, tuna mechi ngumu ya marudiano lakini ninaamini tuna kazi kwenye mechi ya marudiano,”amesema Nadir.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in