Connect with us

 

Uongozi wa klabu ya Yanga FC nchini Tanzania umetangaza kuwa mechi ya Jumanne hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, itakuwa bure.

Mchuano huo utachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, na tayari kikosi cha Mazembe kimeshawasili kutoka mjini Lubumbashi.

Awali, uongozi wa Yanga ulikuwa umetangaza kuwa kiingilio cha chini kushuhudia mchuano huo ilikuwa ni Shilingi 7,000 za Kitanzania.

Mzozo wa mashabiki wa Simba kuweka wazi kuwa wataishangilia TP Mazembe katika mchuano huo huenda imesababisha Yanga FC kuchukua msimamo wa mashabiki wake kuja kwa wingi kwa kuweka mechi hiyo bila ya kulipa chochote.

Hii ni mechi ya pili kwa Yanga FC baada ya kufungwa na MO Bejaia ya Algeria bao 1 kwa 0 huku Mazembe wakiendelea katika mchuano huu baada ya kuapata ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Medeama ya Ghana.

More in