Connect with us

Timu za taifa za mchezo wa soka za wanawake za Zambia, Afrika Kusini, Ghana na Cameroon zimeanza kwa ushindi, michuano ya 11 kuwania taji la bara Afrika.

Fainali hizo zilianza mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Ghana.

Zambia ilipata ushindi mkubwa wa mabao 5-0 na kuwashangaza Equitorial Guinea ambao walilemewa katika mchuano huo wote.

Kabla ya mchuano huo, Equitorial Guinea ilikuwa na mzozo na Kenya, baada ya kuondolewa na kurejeshwa tena katika michuano hiyo kwa madai kumchezesha mchezaji wa taifa lingine.

Matokeo mengine ya kundi B, mabingwa watetezi Nigeria, walilazwa na Afrika Kusini bao 1-0.

Wenyeji Ghana, nao walianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Algeria, huku Cameroon wakiwshinda Mali mabao 2-1.

Siku ya Jumanne, Mali itakabiliana na Ghana, huku Algeria ikicheza na Cameroon.

Mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, wataliwakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia mwaka 2019 jijini Paris nchini Ufaransa.

 

More in AWCON