Connect with us

Zanzibar imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji kwa kuifunga Tanzania Bara Kilimanjaro Stars mabao mawili kwa moja.

Huo ni ushindi wa pili kwa Zanzibar ambayo kwenye mchezo wa kwanza iliitandika Rwanda mabao 3-1.

Kilimanjaro Stars ilimaliza kipindi cha kwanz aikiwa mbele kwa bao lililofungwa na kiungo Himid Mao.

Kipindi cha pili Zanzibar iliyocheza kwa uelewano mkubwa ilisawazisha kupitia Kassim Hamis kabla ya kupata bao la pili lililofungwa na IbrahimAhmada.

Matokeo hayo ni mwendelezo wa matokeo mabovu kwa Stars pindi inapokutana na Zanzibar Heroes kwenye mashindano hayo.

Mwaka 2012 katika mashindano hayo Zanzibar iliishinda Kilimanjaro Stars kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kwa mikwaju 6-5 baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa dakika 90.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in