Connect with us

 

Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Algeria Kheireddine Zetchi amesema kazi yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa katika wadhifa huo ni kurejesha ubora wa timu ya taifa ya soka.

Zetchi alichaguliwa bila kupingwa siku ya Jumatatu baada ya Mohamed Raouraoua, kukataa kuwania kwa muhula wa tatu.

Rais huyo mpya, amesema ana nia ya kumpata kocha mpya wa timu ya taifa kwa muda wa wiki mbili baada ya kujiuzulu kwa George Leekens kutoka Ubelgiji baada ya kuondolewa katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari.

Mbali na kuimarisha timu ya taifa, rais huyo mpya amesema kuwa lengo lake lingine ni kuimarisha soka nchini humo.

Raouraoua, amemaliza muda wake baada ya kuongoza soka nchini humo kwa miaka 12, muda mabao wachambuzi wa soka wanasema alijitahidi sana kuimarisha soka la Algeria kimataifa.

Kawesi alikuwa ni afisa wa kutegemewa sana na ambaye alifanya kazi kwa weledi wa hali ya juu, kitu tunachoweza kujifunza kutoka kwake ni utumishi wake, licha ya kwamba aliishi muda mfupi. Maafisa wa polisi wanastahili kujifunza kuwa, wajitolee kuwatumia wananchi na mambo mengine yote watayapata.

 

More in