Connect with us

Zimbabwe imejiondoa kwenye michuano ya soka kuwania taji la Afrika Mashariki na Kati CECAFA kwa sababu za kiusalama. Michuano hiyo itaanza siku ya Jumapili nchini Kenya.

Zimbabwe ilikuwa imealikwa kushiriki katika michuano hii kutoka Kusini mwa bara la Afrika.

Timu ya taifa ya Libya pia imealikwa kushiriki katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki na Kati.

Shirikisho la soka nchini Zimbabwe limesema kuwa limesikitika kuwa timu yake haitashiriki katika michuano hii lakini itaweza kufanya hivyo katika siku zijazo.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema ratiba ya michuano hiyo itabadilika baada ya Zimbabwe kujiondoa.

Kundi A: Kenya, Rwanda, Libya, Tanzania na Zanzibar

Kundi B: Uganda, Zimbabwe (imejiondoa), Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji Kenya na Rwanda lakini mechi nyingine siku hiyo ya kwanza itakuwa ni kati ya Libya na Tanzania.

IMichuano hiyo itachezwa katika uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega, Afraha Nakuru, Mumias Sports Complex na Moi, mjini Kisumu.

More in East Africa