Connect with us

AFC Leopards yampata kocha mpya

Uongozi wa kllabu ya AFC Leopards nchini Kenya, umemteua Andre Cassa Mbungo raia wa Rwanda kuwa kocha wake mpya, baada ya kujiuzulu kwa Mserbia Marko Vasilejevic kwa sababu ya matokeo mabaya.

Cassa Mbungo mwenye umri wa miaka 51, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, kuisaidia klabu hiyo ambayo inashikilia nafasi ya 15 kati ya 18 kufanya vema katika ligi kuu ya soka nchini humo.

Kocha huyo anakuwa mkufunzi wa 26 wa mabingwa hao wa zamani wa soka nchini humo tangu mwaka 2009, na anakuwa kocha wa sita tangu mwaka uliopita.

Kibarua chake cha kwanza kitakuwa siku ya Jumatano, wakati AFC Leopards itakapochuana na Mount Kenya United.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in