Connect with us

AFCON 2017: DRC yalemewa na Jamhuri ya Afrika ya Kati

AFCON 2017: DRC yalemewa na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipata pigo baada ya kufungwa mabao 2 kwa 0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mechi hiyo ilipigwa jijini Bangui na matokeo hayo yamewashangaza wapenzi wa soka nchini DRC.
Mabao yote ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yalifungwa katika kipindi cha kwanza, huku bao la kwanza likitiwa kimyani katika dakika 27 kupitia mkwaju wa Penalti uliotiwa kimyani  na Vivien Madibe huku  Junior Gourrier akifunga bao la pili na la ushindi.

Leopard sasa ni ya tatu katika kundi lao kwa alama 3 sawa na Jamhuri ya Kati ambao ni wa pili na kundi hilo linaongozwa na Angola ambayo ina alama nne baada ya kutoka sare ya kutofungana na na Madagascar.
Matokeo kamili ya mwishoni mwa juma:

Ijumaa tarehe 4/9/2015
Djibouti 0 Togo 2
Jumamosi 5/9/2015
Comoros 0 Uganda 1
Ushelisheli1 Ethiopia 1
Burundi 2 Niger 0
Namibia 0 Senegal 2
Rwanda 0 Ghana 1
Tanzania 0 Nigeria 0
Boswatana 1 Burkina Faso 0
Sao Tome 0 Morocco 3
Guinea Bissau 2 Congo
Liberia 1 Tunisia 0
Sudan Kusini 1 Equatorial Guinea 0
Mauritani 3 Afrika Kusini 1
Gabon 4 Sudan 0

Jumapili tarehe 6 /9/2015

Mauritius 1 Msumbiji 0 
Madagascar 0 Angola 0
Swaziland 2 Malawi 2
Zimbabwe 1 Guinea 1
Lesotho 1 Algeria 3
Kenya 1 Zambia 2
Jamhuri ya Afrika ya Kati 2 DRC 0
Chad 1 Misri 5
Sierra Leone 0 Cote d'ivoire 0
Benin 1 Mali 1
Gambia 0 Cameroon 1
Libya 1 Cape Verde 2

 

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in