Connect with us

AFCON 2017: Mataifa ya Afrika kujitupa uwanjani

AFCON 2017: Mataifa ya Afrika kujitupa uwanjani

Mwishoni mwa juma hili mashabiki wa soka barani Afrika watakuwa katika viwanja mbalimbali kushuhudia michuano ya makundi kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Afrika Mashariki siku ya Jumamosi, Burundi watakuwa wenyeji wa Niger jijini Bujumbura  huku Uganda Cranes wakiwa ugenini kumenyana na Comoros.

Amavubi Stars ya Rwanda itakuwa nyumbani katika uwanja wa Amahoro  kukipiga na Black Stars ya Ghana. Huu ni mchuano ambao wadadisi wa soka wameuelezea kuwa utakuwa kama vita kati ya Goliath na Daudi.

Mchuano mwingine unachezwa siku ya Jumamosi ni kati ya Tanzania ambao watakuwa nyumbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kumenyana na Super Eagles ya Nigeria.

Mchuano huu ni muhimu kwa makocha wa timu zote mbili ambao wanavinoa vikosi vyao kwa mara ya kwanza katika mashindano haya ya kufuzu.

Kocha wa Tanzania Charles Boniface Mkwasa ataongoza Taifa Stars kutafuta ushindi wake wa kwanza sawa na Sunday Oliseh wa Nigeria.

Tanzania ilikuwa imepiga kambi nchini Uturuki kwa muda wa wiki moja kujiandaa kwa mchuano huu muhimu.

Sudan Kusini pia watachuana na Equatorial Guinea huku Sudan wakiwa ugenini kupambana na Gabon.

Mechi zingine zitakuwa ni kati ya Guinea Bissau dhidi ya Congo Brazaville, Ushelisheli na Ethiopia na Mauritania watawavaa Afrika Kusini nyumbani.

Siku ya Jumapili pia itakuwa ni siku nyingine ya kujitupa viwanjani.

Harambee Stars ya Kenya itakuwa katika uwanja wake wa kihistoria wa Nyayo jijini Nairobi kupambana na mabingwa wa mwaka 2012 Chipolopolo ya Zambia.

Zambia inasema inaiheshimu Kenya na inatarajia mchuano mgumu jijini Nairobi.

Rais wa Shirikisho la soka nchini humo Sam Nyamweya amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono Stars.

Nayo Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa ugenini kupambana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jijini Bangui.

Swaziland watacheza na Malawi, Zimbabwe dhidi ya Guinea huku Chad wakimenyana na Misri jijini Djamena.

Gambia nao wataivaa Cameroon huku Libya wakiwa wenyeji wa Cape verde.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in