Connect with us

 

Kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Gernot Rohr ameanza kukiandaa kikosi cha Super Eagles kuelekea mchuano wa mwisho dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania, kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Gabon.

Huu utakuwa ni mchuano wa kwanza chini ya kocha huyu raia wa Ujerumani, na utachezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Akwa Ibom katika jimbo la Uyo.

Kikosi cha wachezaji wa kulipwa wa Nigeria wakiongozwa na nahodha Mikel John Obi na naibu wake Ahmed Musa, tayari wameshawasili na kuanza mazoezi.

Wachezaji wengine ni pamoja na Makipa: Emmanuel Daniel na Ikechukwu Ezenwa.

Mabeki: Musa Muhammed, Chidozie Awaziem, Abdullahi Shehu, Jamiu Alimi, Leon Balogun, William Troost-Ekong na Elderson Echiejile.

Viungo wa Kati:Ogenyi Onazi, Wilfred Ndidi na Nosa Igiebor.

Washambuliaji: Brown Ideye, Imoh Ezekiel, Kelechi Iheanacho, Victor Moses, Odion Ighalo na Victor Osimhen.

Timu ya taifa ya Tanzania inawasili siku ya Jumatano ikiongozwa na kocha Charles Bonface Mkwasa.

Mchuano kati ya mataifa haya mawili hautakuwa na maana yeyote kuelekea katika fainali ya Gabon kwa sababu , mataifa yote mawili yameshaondolewa.

Misri ndio taifa lililofuzu katika hatua hii.

More in East Africa