Connect with us

AFCON 2017: Tanzania yadhamiria kuinyamazisha Nigeria

AFCON 2017: Tanzania yadhamiria kuinyamazisha Nigeria

Mashabiki wa soka Afrika Mashariki wanajiuliuliza ikiwa Nigeria itaendeleza rekodi yake ya kuzilemea timu za Afrika Mashariki katika michuano ya Kimataifa.

Tanzania wanawakaribisha Nigeria Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchuano wa makundi kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Mataifa yote yana makocha wapya, Nigeria chini ya Sunday Oliseh na Tanzania chini ya Charles Boniface Mkwasa.

Oliseh amesema kuwa Nigeria inaiheshimu Tanzania na vijana wake watapambana huku Mkwasa akisema wachezaji wake wako tayari kucheza kufa kupona.

Kikosi cha Tanzania:

Makipa: Ali Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) and Said Mohamed (Mtibwa Sugar)

Mabeki: Shomari Kapombe (Azam FC), Abdi Banda, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba SC), Juma Abdul, Haji Mngwali, Kelvin Yondani and Nadir Haroub (Yanga).

Viungo wa Kati: Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo (Azam FC), Salum Telela, Deus Kaseke (Yanga), Said Ndemla (Simba SC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe)

Washambuliaji: John Bocco, Farid Musa, (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Simon Msuva (Yanga SC), Ibrahim Ajib (Simba). Mbwana Samatta, , Mrisho Ngassa (Free State Stars)

Kikosi cha Nigeria:

Makipa: Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England); Femi Thomas (Enyimba FC, Nigeria); Ikechukwu Ezenwa (Sunshine Stars, Nigeria)

Mabeki: Leon Balogun (FSV Mainz 05, Germany); Kingsley Madu (AS Trencin, Slovakia); Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Turkey); William Troost Ekong (FK Haugesund, Norway); Kenneth Omeruo (Kasimpasa SK, Turkey); Solomon Kwambe (Warri Wolves); Chima Akas (Sharks FC, Nigeria)

Viungo wa Kati: Izunna Ernest Uzochukwu (FC Amkar Perm, Russia); Obiora Nwankwo (Coimbra FC, Portugal); Lukman Haruna (Anzhi Machatsjkala, Russia); Rabiu Ibrahim (AS Trencin, Slovakia); Usman Mohammed (FC Taraba, Nigeria); Austin Obaroakpo (Abia Warriors, Nigeria)

Washambuliaji : Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Emem Eduok (Esperance ST, Tunisia); Emmanuel Emenike (Al Ain, UAE); Anthony Ujah (Werder Bremen, Germany); Sylvester Igboun (FC UFA, Russia); Moses Simon (KAA Gent, Belgium); Prince Aggrey (Sunshine Stars, Nigeria)

Historia ya michuano zilizopita kati ya Tanzania na Nigeria

06 Julai 1972 Tanzania 0 v Nigeria 0

12 Januari 1973 Nigeria 2 v Tanzania 1

08Machi 1980 Nigeria 3 v Tanzania 1

06 Desemba 1980 Nigeria 1 v Tanzania 1

20 Desemba 1980 Tanzania 0 v Nigeria 2

11 Septemba 2002 Nigeria 2 v Tanzania 0

Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuuz katika michuanoya Afrika ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria.

 

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in