Connect with us

Ahcene Ait-Abdelmelek raia wa Ujerumani mwenye asili ya Algeria, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Sudan Kusini.

Ait-Abdelmelek atawasili jijini Juba tarehe tano mwezi Machi kuanza kuifunza Bright Stars.

Imeripotiwa kuwa mshahara wake utakuwa ni Dola za Marekani 5,000 kila mwezi.

Anachukua nafasi ya kocha Bilal Felix ambaye amekuwa akikaimu kama Kocha wa timu ya taifa.

Kazi kubwa ya kocha huyu mpya ni kuisaida Sudan Kusini kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Bright Stars wamepangwa pamoja na Burundi, Mali na Gabon katika kundi C

More in East Africa