Connect with us

 

Shirikisho la soka nchini Rwanda limemtangaza rasmi Mjerumani Antoine Hey kuwa kocha mpya wa Amavubi Stars, na kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Hey aliteuliwa mwezi uliopita kuifunza Rwanda, baada ya kuwashinda makocha wengine zaidi ya 50 waliokuwa wameomba kazi ya kuifunza nchi hiyo.

Rais wa FERWAFA Vincent Nzamwita amesema kazi kubwa ya Hey, itakuwa ni kwa Rwanda kufuzu katika fainali ya kombe la bara Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon na michuano ya CHAN mwaka 2018 nchini Kenya.

Kocha huyo ambaye amewahi kufunza soka nchini Kenya, Gambia na Lesotho amesema anatambua kazi kubwa iliyo mbele yake.

”Tuna ratiba ngumu mbele yetu, kwa muda wa miezi sita ijayo tutakuwa na mechi kadhaa za kucheza kufuzu katika fainali za AFCON na CHAN, hatuna muda wa kupoteza,” amesema Hey.

Rwanda itapambana na Cote d’Ivoire, Guinea na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika michuano ya kufuzu kwa fainali ya AFCON mwaka 2019.

Mbali na michuano hiyo ya AFCON, Rwanda itapambana na Tanzania mwezi Julai katika mchuano wa kufuzu kucheza fainali ya CHAN.

 

More in