Connect with us

Burkina Faso kumenyana na Nigeria fainali ya michezo ya Afrika

Burkina Faso kumenyana na Nigeria fainali ya michezo ya Afrika

Timu ya taifa ya soka ya Burkina Faso yenye wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 imefuzu katika fainali ya michezo ya Afrika iliyoendelea jijini Congo Brazaville.

Vijana wa Burkina Faso waliwashangaza Nigeria kwa kuwafunga mabao 3 kwa 1 katika nusu fainali ya kusisimua siku ya Jumanne jioni.

Sydney Mohamed Sylla aliipatia Burkina Faso bao la kwanza katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo baada ya Nigeria kukosa nafasi nyingi za kutikisa nyavu

Omar Kabore naye alihakikisha kuwa timu yake inapata ushindi katika kipindi cha pili kwa kufunga bao muhimu kabla ya Nigeria kupata bao la kufuta machozi.

Katika mchuano mwingine wa nusu fainali, Senegal waliwashinda wenyeji wa mashindano hayo Congo Brazaville kwa mabao 3 kwa 1.

Burkina Faso itachuana na Sengal katika fainali itakayochezwa siku ya Ijumaa.

Kwa upande wa wanawake, Ghana na Cameroon watamenyana kupata medali ya dhahabu katika mchezo wa fainali pia siku ya Ijumaa.

Black Queens ya Ghana ilifunzu baada ya kuifunga Les Elephantes ya Cote d’Ivoire bao 1 kwa 0 huku Le Lioness ya Cameroon ikiishinda Super Falcons ya Nigeria mabao 2 kwa 1.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in