Connect with us

CAF: Al Merrikh na Al Hilal zafuzu nusu fainali klabu bingwa

CAF: Al Merrikh na Al Hilal zafuzu nusu fainali klabu bingwa

Sudan itawakilishwa na vlabu viwili katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika msimu huu.

Al Merrikh na Al Hilal zilifuzu katika hatua hiyo baada ya kumalizika kwa michuano ya makundi mwishoni mwa juma lililopita.

Vlabu vingine vilivyofuzu ni mabingwa wa mwaka 2010 TP Mazembe ya DRC na USL Alger ya Algeria.

Al Merrikh itapambana na TP Mazembe katika nusu fainali ya mzunguko wa kwanza mwisho wa mwezi wa Septemba jijini Khartoum kabla ya kukutana tena katika mchuano wa mzunguko wa pili mjini Lubumbashi mapema mwezi Oktoba.

Mazembe wamefuzu katika hatua hii baada ya ushindi mkubwa wa mabao 5 kwa 0 dhidi ya Moghreb Tetoun ya Morroco mwishoni mwa wiki iliyopita na kumaliza kundi la A kwa alama 11, mbele ya Al Hilal iliyokuwa na alama 9 baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 na Smouha ya Misri.

USM Alger waliongoza kundi la B kwa alama 15 mbele ya Al -Merrikh iliyomaliza kwa alama 13.

Mabingwa watetezi wa taji hili ES Setif walibanduliwa nje ya mashindano haya baada ya kushindwa kufuzu kwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 5.

Kuhusu michuano ya Shirikisho, Al-Ahly na Zamalek zote kutoka Misri pia zimefuzu katika hatua hiyo ya nusu fainali sawa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Orlando Pirates itamenyana na Al-Ahly huku Etoile du Sahel ikichuana na Zamalek.

Zamalek walimaliza mchuano wa makundi kwa kupata ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa 1 na kumaliza kundi lake la A kwa alama 15 ikifuatwa na Orlando Pirates iliyomaliza kwa alama 12.

Al-Ahly nayo ilimaliza kundi lao la A kwa alama 13 na mwishoni mwa juma ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Stade Malien ya Mali huku Etolile du Sahel iliyomaliza ya pili kwa alama 13 pia ikiwachabanga Esperance de Tunis kwa mabao 2 kwa 1.

Nusu fainali itachezwa nyumbani na ugenini.

 

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in