Connect with us

CAF CL: Yanga yaondolewa na Zesco,Koro amekiri wanarudi kujipanga

CAF CL: Yanga yaondolewa na Zesco,Koro amekiri wanarudi kujipanga


Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Kocha Mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera baada ya kuondolewa
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika amekiri kuwa kwa sasa
wanarudi nyumbani na kikosi chake kujipanga katika michezo ya Ligi
Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/2020 huku wakisubiri shirikisho
la soka Afrika CAF litawapanga na timu gani katika kuwania kufuzu
kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho
Afrika.

Kwanza tunarudi nyumbani (Tanzania) kujiandaa na Ligi na Kombe
la shirikisho sasa tunangoja kujua ni nani tutacheza nae ndio tufanye
maandalizi ya kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano ya
Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup)” alisema kocha mkuu
wa Yanga Mwinyi Zahera kupitia Azam TV.

Yanga imeondolewa katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na
Zesco ya Zambiwa wakiwa katika uwanja wa Levy Mwanawasa Ndola
Zambia, baada ya dakika ya 78 wakiwa wanaamini kuwa wataenda
hatua ya mikwaju ya penati kwani hadi dakika hiyo walikuwa 1-
1(Agg 2-2), kwa goli lililofungwa na Sadney dakika ya 30 baada ya
Jesse Were kufunga goli la uongozi kwa Zesco dakika ya 24 ila kwa
bahati mbaya Makame wa Yanga akajifunga na kumaliza safari ya
Yanga, hivyo dakika 90 zikamalizika ikiwa 2-1 (Agg 3-1)

Tanzania kwa sasa haina muwakilishi yoyote katika michuano ya Ligi
ya Mabingwa Afrika baada ya Yanga kutolewa na Simba kutolewa
hatua ya mapema zaidi na ukizingatia Azam FC nao wametolewa na
Triangle FC ya Zimbabwe katika michuano ya Kombe la shirikisho
Afrika, Tanzania msimu huu inabakia na Yanga pekee kama
muwakilishi wa michuano ya kimataifa (Kombe la Shirikisho)
ambaye nae ameangukia michuano hiyo baada ya kutolewa na Zesco.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in