Connect with us

CAF: Etoile du Sahel yalazimisha sare na Orlando Pirates

CAF: Etoile du Sahel yalazimisha sare na Orlando Pirates

Klabu ya soka ya Orlando Pirates kutoka Afrika Kusini, ilifungwa na Etoile du Sahel ya Tunisia katika dakika za lala salama na kusawazisha bao la mapema walilokuwa wamefunga katika fainali ya kwanza ya kuwani taji la Shirikisho barani Afrika siku ya Jumamosi usiku.

Afrika Kusini ilichukua uongozi wa mchuano huo katika dakika 36 baada ya kupata bao kupitia shuti safi la mchezaji Thamsanqa Gabuza.

Bao la kusawazisha la Etoile du Sahel lilitiwa kimyani katika dakika ya 87 kipindi cha pili, kupitia Ammar Jemal.

Etoile du Sahel wamerudi nyumbani na bao la ugenini ambalo ni muhimu sana kuelekea fainali ya pili.

Fainali ya mwisho itachezwa siku ya Jumapili tarehe 29 mwezi huu katika uwanja wa Olympique jijini Tunis.

Mshindi pamoja na kupata kombe atapata tikita cha Dola za Marekani 660,000.

Aidha, bingwa atamenyana na bingwa wa klabu bora barani Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo katika fainali ya kuwania taji la Super Cup.

 

Must See

More in