Connect with us

CAF: TP Mazembe kuvaana na USM Alger fainali ya kwanza

CAF: TP Mazembe kuvaana na USM Alger fainali ya kwanza

Klabu ya soka ya USM Alger kutoka Algeria siku ya Jumamosi inachuana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika fainali ya kwanza ya klabu bingwa barani Afrika CAF mwaka 2015.

Mshindi atanyakua zawadi ya kitita cha Dola Milioni 1 nukta 5 na kufuzu katika fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu itakayofanyika nchini Japan mwezi Desemba.

Fainali hii inatarajiwa kuwa ngumu na ya kusisimua na USM inafika katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza, huku TP Mazembe wakiwa na uzoefu baada ya kushinda taji hilo mara nne mwaka 1967, 1968, 2009 na 2010.

Kikosi cha USM Algier kinaongozwa na kocha Miloud Hamdi, na wachezaji wake wengi ni wa nyumbani wakiwemo, Zinedine Ferhat na Mohamed Meftah bila kumsahau mshambuliaji wa Carolus Andriamanitsinoro.

Mazembe inayofunzwa na kocha Patrice Cateron kutoka Ufaransa inawashirikisha wachezaji wa nyumbani Ghana, Ivory Coast, Mali, Tanzania na Zambia.

Miongoni mwa wachezaji wa kuangaliwa katika kikosi cha TP Mazembe ni pampja na kipa maarufu Robert Kidiaba, Rainford Kalaba kutoka Zambia na Mbwana Samatta kutoka nchini Tanzania.

Hadi kufika katika hatua ya fainali, USM Algier ilishinda mechi zake zote sita katika hatua ya makundi na kufunga mabao 14.

TP Mazembe nayo ilifanya vizuri nyumbani na kufungwa mechi nyingi za ugenini huku akipata ushindi katika mchuano mmoja wa ugenini.

Fainali ya ili itachezwa tarehe 8 mwezi Novemba.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in