Connect with us

CAF: Vlabu vya Afrika Mashariki vyaanza vibaya

CAF: Vlabu vya Afrika Mashariki vyaanza vibaya

Klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Mafunzo FC ya Zanzibar na APR ya Rwanda zote zimeanza vibaya michuano ya soka hatua ya awali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika CAF mwaka 2016.

Mafunzo FC ikiwa nyumbani ilifungwa na AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mabao 3 kwa 0.

Nao mabingwa wa Kenya Gor Mahia wakicheza nyumbani katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi,nao walifungwa mabao 2 kwa 1 na klabu ya CNAPS Sport ya Madagascar.

Mbabane Swallows wa Swaziland, wakiwa nyumbani mjini Mbabane, nao waliifunga APR ya Rwanda bao 1 kwa 0.

Vipers FC ya Uganda ikicheza katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala, iliifunga Enyimba ya Nigeria 1 kwa 0.

Vipers wanashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza, ikilinganishwa na ambayo ina uzoefu wa michuano hii na hata kunyakua ubingwa mwaka 2003 na 2004.

Yanga ya Tanzania, nayo ikicheza ugenini dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius, ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0.

Matokeo ya michuano ya Shirikisho CAF

  • Police (Rwanda) 3 vs Atlabara (Sudan Kusini) 1
  • FC Saint Eloi Lupopo ( DRC) 2 vs Bandari (Kenya) 0
  • Khartoum (Sudan) 0 vs SC Villa (Uganda ) 1
  • JKV (Zanzibar ) 3 vs Gaborone United ( Boswatana ) 0, baada ya Gaborone FC kutofika Zanzibar
  • Fomboni Club (Comoros ) 1 vs Atletico Olympic (Burundi) 0

Michuano ya marudiano itachezwa baadaye mwezi huu na mshindi kufuzu katika hatua ya kwanza ya michunao hii ya Shirikisho na klabu bingwa.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in