Connect with us

CECAFA 2015: Sare yaisaidia Ethiopia kufuzu robo fainali

CECAFA 2015: Sare yaisaidia Ethiopia kufuzu robo fainali

Mataifa nane yaliyofuzu katika hatua ya robo fainali kuwania taji la CECAFA, katika eneo la Afrika Mashariki na Kati ni pamoja na Tanzania, wenyeji Ethiopia, Rwanda , Kenya, Uganda, Sudan, Malawi na Sudan Kusini.

Jumapili ni siku ya mapumziko kabla ya kuanza kabla ya michuano ya robo fainali siku ya Jumatatu.

Ratiba

Jumatatu tarehe Novemba 30 2015

Uganda vs Malawi
Tanzania vs Ethiopia

Jumanne Desemba 1 2015

South Sudan vs Sudan
Kenya vs Rwanda

Wenyeji Ethiopia walipata bao muhimu katika dakika za lala salama baada ya mabeki wa Tanzania bara kujichanganya na kujifunga.

Ethiopia ambayo ilimaliza ya tatu katika kundi la A kwa alama 4, ilihitaji bao moja tu kufuzu mbele ya Burundi.

Mapema katika mchuano mwingine, Uganda iliifunga Burundi bao 1 kwa 0 na kuiweka Intamba Murugamba katika nafasi ngumu ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali.

Mchuano mwingine unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya Sudan Kusini na Sudan.

Timu hizi mbili zilikutana katika hatua ya makundi na kutoka sare ya kutofungana.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in