Connect with us

CECAFA 2015: Ethiopia, Uganda, Rwanda na Sudan kusaka kufuzu fainali

CECAFA 2015: Ethiopia, Uganda, Rwanda na Sudan kusaka kufuzu fainali

Hatua ya nusu fainali kuwania ubingwa wa mwaka 2015 katika  mchezo wa soka baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA inachezwa leo Alhamisi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mchuano wa kwanza unawakutanisha mabingwa wa mwaka 2006 Sudan dhidi ya Amavubi Stars ya Rwanda.

Mwaka 2006 wakati michuano hii ilipoandaliwa tena nchini Ethiopia, Sudan walifika katika hatua ya nusu fainali na baadaye kufuzu hadi fainali na kuwashinda wageni Zambia kupitia mikwaju ya penalti.

Licha ya kufungwa na Malawi mabao 2 kwa 1 na kutoka sare ya kutofungana na jirani yake Sudan Kusini, Falcon FC wamejikakamua na kufika katika hatua ya nusu fainali.

Mara ya mwisho Sudan kufika katika hatua ya fainali katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2013 wakati mashindano haya yalipofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na wenyeji Harambee Stars kuibuka mabingwa.

Rwanda nayo mara ya mwisho kufika fainali ilikuwa ni mwaka 2009.

Kocha wa Amavubi Stars John McKinstry ameweka matumaini yake kwa wachezaji kama  Jacques Tuyisenge na Haruna Niyonzima ambao wameonekana kuchangia mafanikio kwa timu yao.

Ethiopia vs Uganda

Huu ni mchuano utakaowavutia mashabiki wengi kwa sababu Ethiopia wako nyumbani.

Uganda pia inaangaziwa kwa karibu na kila mmoja kutokana na rekodi yake nzuri ya kunyakua mataji 13 ya CECAFA.

Cranes wanaofunzwa na kocha Milutin Micho Sredojevic wanalenga kuwashinda wenyeji na kufika fainali kulisaka taji la 14 kurudi nalo jijini Kampala.

Uganda walianza vibaya baada ya kufungwa na watani wao wa jadi Kenya mabao 2 kwa 0 lakini wakaedelea kuandkisha matokeo mazuri, dhidi ya Zanzibar na Burundi katika kundi lao.

Mara ya mwisho mataifa haya kukutana ilikuwa ni mwezi Novemba mwaka jana , mchuano ambao Uganda waliibuka washidi kwa kupata mabao 3 kwa 0 jijini Kampala.

Hadi kufika katika hatua ya nusu fainali,  Ethiopia kwa jina maarufu kama Walia Ibex walianza vibaya kwa kufungwa na Rwanda bao 1 kwa 0 lakini baadaye wakashinda Somalia mabao 2 kwa 0 na kufuzu baada ya sare ya bao 1 kwa 1 na Tanzania bara na baadaye kukutana tena na Kilimanjaro Stars katika hatua ya robo fainali  na kuwashinda kupitia mikwaju ya penalti.

Kocha wa Yohannes Sahle amewaambia wachezaji wake kucheza kwa nguvu dakika zote 90 na kutafuta mabao ya mapema dhidi ya Uganda timu ambayo anakiri ni nzuri.

Uganda Cranes na  Ethiopia Walia ibex wamekutana mara 35 katika michuano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo 10 ya CECAFA.

Uganda wameshinda mara 14 na Ethiopia mara 13 na kutoka sare mara nane.

Washindi katika nusu fainali zote watamenyana katika mchuano wa fainali siku ya Jumamosi jijini Addis .

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in