Connect with us

 

Timu ya taifa ya soka ya Kenya itamenyana na Ethiopia katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la CECAFA kwa upande wa wanawake, katika michuano inayoendelea katika taasisi ya kukuza soka ya Njeru mjini Jinja nchini Uganda.

Katika mchuano mwingine, wenyeji Uganda watamenyana na Tanzania bara.

Michuano hii yote utapigwa siku ya Jumapili, huku fainali ikichezwa siku ya Jumanne wiki ijayo.

Siku ya Jumamosi ni siku ya mapumziko.

Harambee Starlets ya Kenya ilifuzu baada ya kushinda mechi zake zote za kundi A, na kutofungwa bao lolote.

Hivi ndivyo matokeo yalivyokuwa:

Kenya 4-0 Uganda

Kenya 4-0 Burundi

Kenya 11-0 Zanzibar

Uganda nayo ilimaliza ya pili katika kundi hili la A:

Uganda 0-1 Kenya

Uganda 9-0 Zanzibar

Uganda 1-0 Burundi

Kilimanjaro Queens ya Tanzania bara nayo ilifuzu huku mchuano wake wa mwisho dhidi ya Lucy ya Ethiopia ikimalizika kwa sare ya kutofungana.

Matokeo ya Tanzania katika michuano hii:-

Tanzania 3-2 Rwanda

Tanzania 0-0 Ethiopia

Ethiopia nayo ilifuzu baada ya kmaliza ya pili katika kundi B kwa alama nne baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-2.

 

More in East Africa