Connect with us

CHAN 2016: Guinea yatoka sare na Tunisia

CHAN 2016: Guinea yatoka sare na Tunisia

Timu ya taifa ya soka ya Guinea inayoshiriki katika michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN inayoendelea nchini Rwnada, ilitoka nyuma na kusawazisha mabao 2 waliyokuwa wamefungwa na Tunisia katika mchuano wa Kundi C.

Mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali ulimalizika kwa timu zote mbili kufungana mabao 2 kwa 0.

Tunisia ilianza kupata bao katika dakika ya 33 kipindi cha kwanza na Ahmed Akaïchi na baadaye Alseny Camara Agogo kuisawazishia Guinea katika dakika 40.

Kipindi cha pili timu zote mbili ziliendeleza mashambulizi na katika dakika ya 51, Akaichi aliifungia tena Tunisia katika dakika ya 51, huku Agogo akiisawazishia timu yake katiak dakika 83.

1160422_full-lnd Tunisia

Mchuano mwingine wa kundi hili kuanzia saa moja jioni saa za Afrika ya Kati ni kati ya Niger na Nigeria.

Kesho Jumnne, itakuwa ni zamu ya kundi la D, Zimbabwe itachuana na Zambia, na baadaye Mali watamenyana na Uganda.

Mechi hizi zitapigwa katika uwanja wa Umuganda katika mji wa Gisenyi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in