Connect with us

CHAN 2016: Rwanda yasema iko tayari kwa michuano ya CHAN

CHAN 2016: Rwanda yasema iko tayari kwa michuano ya CHAN

Rwanda inaingia katika vitabu vya kihistoria kwa kuandaa mashindano makubwa ya soka barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani CHAN, kuanzia Jumamosi hii.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya kufanyika nchini Rwanda na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kat,i tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2009 nchini Cote D’voire.

Serikali ya Rwanda kupitia Wizara ya michezo imesema nchi hiyo iko tayari kwa mashindano hayo yatakayomalizika tarehe 7 mwezi Februari.

Michuano hiyo itachezwa katika miji mitatu, jiji kuu Kigali na miji ya Gisenyi na Butare.

Viwanja vitakavyotumiwa katika mashindano hayo ni pamoja na ule wa Amohoro na Nyamirambo vyote vilivyo jijini Kigali, uwanja wa Huye mjini Butare na ule wa Umuganda huko Gisenyi.

Serikali ya Rwanda inasema imetumia Dola Milioni 21 nukta 4 kuandaa makala haya ya nne ya CHAN.

Idadi kubwa ya mashabiki kutoka katika mataifa 15 yanayoshiriki katika michuano hii wanatarajiwa kushuhudia mashindano hayo baada ya serikali kuondoa ada ya Visa kwa wageni watakaopenda kwenda nchini Rwanda.

Mataifa 16 yanayoshiriki katika michuano hii ni pamoja na:- Kundi A Gabon, Ivory Coast, Morocco na wenyeji Rwanda.

Angola, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ethiopia wanaunda kundi la B.

Kundi C kuna Guinea, Niger, Nigeria na Tunisia huku kundi la D likiwa na Mali, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Mchuano wa ufunguzi ni kati ya wenyeji Amavubi Stars na Tembo kutoka Ivory Coast.

Licha ya Ivory Coast kuwa wneyeji wa michuano hii mwaka 2009, Sudan walikuwa wenyeji mwaka 2011 huku Afrika Kusini ikiwa mwenyeji mwaka 2014.

Kenya itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka 2018.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in