Connect with us

CHAN:Micho akitaja kikosi cha wachezaji 25 kujiandaa dhidi ya Sudan

CHAN:Micho akitaja kikosi cha wachezaji 25 kujiandaa dhidi ya Sudan

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uganda Milutin ‘Micho’ Sredojevic, amekitaja kikosi cha wachezaji 25 wanaocheza soka nyumbani kuanza maandalizi ya mzunguko wa mwisho wa kufuzu michuano wa CHAN dhidi ya Sudan.

Mchuano huo utachezwa jijini Kampala tarehe 17 mwezi huu wa Oktoba na jijini Khartoum tarehe 24.

Kikosi hicho kitaanza maandalizi siku ya Jumanne kuanzia saa nne asubuhi.

Mchuano huo wa mzunguko wa kwanza utachezwa katika uwanja wa Nakivubo na mshindi baada ya mizunguko yote miwili atafuzu katika michuano hiyo ya CHAN itakayofanyika mwaka 2016 nchini Rwanda.

Kikosi Kamili:

Makipa: Kigonya Mathias (Bright Stars FC), Watenga Isma (Vipers Sc), Alitho James (Vipers SC).

Mabeki: Okot Denis (KCCA FC), Kiyemba Ibrahim (LwezaFC), Ochaya Joseph (KCCA FC), Muleme Isaac (SC Villa Jogoo),

Bakaki Shafiq (Vipers SC), Wasswa Hassan Dazo (KCCA FC), Kizza Ayub (Express FC), Muwanga Bernard (Bright Stars FC), Awanyi Timothy (KCCA FC), Katongole Henry (SC Villa Jogoo).

Viungo wa Kati: Ntege Ivan (KCCA FC), Bukenya Deus (Vipers SC), Katumba Peter (Sadolin Paints FC), Senkumba Hakim (KCCA FC), Mutyaba Muzamil (KCCA FC), Kizito Keziron (Vipers SC), Miya Faruku (Vipers SC).

Washambuliaji: Robert Ssentongo (URA FC), Okhuti Caesar (Express FC), Kalanda Frank (URA FC), Sekisambu Erisa (Vipers SC) and Ssemazi John (Vipers SC).

 

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in