Connect with us

Cuthbert Dube ajiuzulu uongozi wa Shirikisho la soka Zimbabwe

Cuthbert Dube ajiuzulu uongozi wa Shirikisho la soka Zimbabwe

Rais wa Shirikisho la soka nchini Zimbabwe ZIFA Cuthbert Dube amejiuzulu. Hatua hii imekuja wakati wajumbe wa soka nchini humo wakikutana siku ya Jumamosi katika Mkutano Mkuu wa soka na ajenda kubwa ilikuwa ni kupiga kura ya kukosa imani na kiongozi wao.

Dube amekuwa akiongoza soka nchini Zimbabwe kwa miaka mitano sasa na wakati wa uongozi wake, deni la Shirikisho hilo limeongezeka na kufikia Dola Milioni 6 na wachezaji wa timu za taifa wanaume na wanawake wamekuwa wakilalamikia malipo na safari zao kutatizika wanapokuwa na ziara nje ya nchi kutokana na uhaba wa fedha.

Wadau wa soka nchini humo wanajadiliana pia kuhusu uchaguzi wa tarehe 5 mwezi Desemba na wawakilishi wa Shirikisho la soka duniani FIFA na CAF wanashiriki.

Hata, hivyo Dube amesema kuwa ataendelea kusalia madarakani hadi viongozi wapya watakapochaguliwa.

Matatizo ya kifedha yameifanya FIFA kuizuia Zimbabwe kushiriki katika michuano ya kufuzu katika dimba la kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya kushindwa kumlipa kocha wake wa zamani wa timu ya taifa Mbrazil Valinhos Dola za Marekani 67,000.

Kocha wa zamani Tom Saintfiet pia amepeleka malalamishi yake kwa FIFA baada ya kutolipa fedha zake alipokuwa mkufunzi mwaka 2010. Saintfiet kwa sasa ni kocha wa Togo.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in