Connect with us

Duarte apewa tena kibarua cha kuifunza Burkina Faso

Duarte apewa tena kibarua cha kuifunza Burkina Faso

Paulo Duarte ameajiriwa tena kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka ya Burkina Faso.

Duarte raia wa Ureno, anachukua nafasi ya Gernot Rohr aliyerejea nyumbani nchini Ujerumani wiki iliyopita kwenda kufanya kazi na Shirikisho la soka nchini Ujerumani.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, aliwahi kuwa kocha wa Stallions kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mara mbili.

Burkina Faso mwaka 2010 na 2012 wakati ikifunzwa na Duarte ilifika katika hatua ya makundi katika fainali ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika.

Kazi kubwa ya kicha huyo itakuwa ni kuisaidia Burkina Faso kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2016 nchini Gabon.

Kipimo cha kwanza kitakuwa ni kati ya Uganda nyumbani mwezi Machi mwaka 2016.

Stallions iko katika kundi D na ni ya tatu kwa alama 3 baada ya kucheza michuano miwili.

Kocha huyo pia amewahi kuifunza Gabon mwaka 2012 na hivi karibuni alikuwa kocha wa CS Sfaxien ya Tunisia kabla ya kuondoka mwezi Agosti mwaka huu.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in