Connect with us

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Ghana, na Makamu rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Kwesi Nyantakyi, amefungiwa maisha na Shirikisho la soka duniani FIFA, kutojihusisha na masuala ya soka katika muda wake wa maisha.

Hatua hii imefikiwa baada ya FIFA, kubaini kuwa alihusika na rushwa baada ya kuonekana alipokea Dola 65,000 kutoka kwa Mwanahabari aliyekuwa anafanya uchunguzi kuhusu suala la ufisadi katika mchezo wa soka.

Mbali na adhabu hiyo kali, Nyantakyi ametozwa faini ya Franca za Uswisi 500,000.

Nyantakyi, alijiuzulu mwezi Juni baada ya kuonekana kwa ripoti ya uchunguzi iliyotolewa na Mwanahabari Anas Aremeyaw Anas akionekana akipokea rushwa, madai ambayo aliyakanusha. Haijafahamika iwapo atakataa rufaa.

More in West Africa