Connect with us

FIFA yampiga marufuku ya maisha Jack Warner

FIFA yampiga marufuku ya maisha Jack Warner

Shirikisho la soka duniani FIFA, limempiga marufuku ya maisha aliyekuwa wakati mmoja Makamu wa rais Jack Warner kutoshiriki katika maswala ya soka. 

Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya maadili ya FIFA, baada ya kubainika kuwa Warner alihusika na maswala mbalimbali ya utovu wa nidhamu.

Kamati hiyo imempata na kosa Warner mwenye umri wa miaka 72 ambaye pia aliwahi kuwa rais wa Shirikisho la soka katika nchi za Amerika ya Kati, Kaskazini na nchi za Carribean CONCAF, alitoa, kupokea fedha zinazoaminiwa ni rushwa mara kwa mara wakati akiwa uongozini.

Warner pia amekuwa akitafutwa na viongozi wa mashtaka nchini Marekani kufunguliwa mashtaka ya kuhusika na ufisadi,tuhma ambazo ameendelea kuzikanusha.

Mohamed Bin Hamman rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Qatar naye alipigwa marufuku ya maisha ya kutoshiriki katika maswala ya soka duniani kwa makosa ya kinidhamu.

Kutokana na tuhma za ufisadi zinazoendelea kuwasonga viongozi wa FIFA akiwemo rais Sepp Blatter, kumekuwa na wito wa kuundwa kwa Kamati maalum ya kusimamia maswala ya soka duniani.

Blatter alichunguzwa na maafisa nchini Uswizi juma lililopita kuhusika tuhma hizi za ufisadi lakini tayari ametangaza kuwa anajiuzulu na uchaguzi utafayika mwezi Februari mwaka jana.

Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcker naye amesimamishwa kazi kwa tuhma za ufisadi.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in