Connect with us

FIFA:Blatter asisitiza hana kosa

FIFA:Blatter asisitiza hana kosa

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA kwa mara nyingine amesisitiza kuwa hatajiuzulu kabla ya tarehe 26 mwezi Februari mwaka ujao wakati uchaguzi mwingine utakapofanyika.

Nitaacha tu kufanya kazi tarehe 26, sio kabla ya siku hiyo,” Blatter ameliambia Jarida la Ujerumani Bunte.

“Nitapambana hadi tarehe 26.Kwa binafsi yangu.Na kwa FIFA.”

Blatter amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kujiuzulu kutokana na tuhma za ufisadi ambazo anakanusha kuhusika.

Aidha, amesisitiza kuwa hana hofu kuhusu uchunguzi unaofanywa na viongozi wa mashtaka nchini Uswizi .

Huu ni uchunguzi tu wa kawaida. Sijafunguliwa mashtaka. Sitashirikiana na maafisa hao,” Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesisitiza.

Wiki iliyopita, wafadhili wa FIFA Coca-Cola, McDonald’s, Visa na Budweiser walimtaka Blatter ajiuzulu kwa kile walichokisema mabadiliko yanaweza kufanyika tu ikiwa ataondoka.

Hata hivyo, Blatter amesema kuwa wafadhili wengine wa kutengeza jezi Adidas, Hyundai na Gazprom kutoka Urusi wamesimama naye na wanamuunga mkono.

Mbali na Blatter, rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Mitchel Platini amesisitiza kuwa hana cha kuficha kuhusu Dola Milioni 2 alizolipwa na FIFA.

Viongozi wa mashtaka nchini Uswizi wanasema alipokea fedha hizo kwa njia zisizoeleweka na kumtuhumu kuhusika na ufisadi.

Kamati ya nidhamu inakutana kuwajadili Sepp Blatter na Mitchel Platini.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in